Na ukiwauliza: Nani aliye ziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu. Wewe sema: Alhamdulillahi! Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wao hawajui. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na lau unawauliza, ewe Mtume, hawa wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, «Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?» Watasema, «Ni Mwenyezi Mungu.» Basi wanaposema hilo, waambie, «Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu Aliyeonyesha ushahidi kutoka kwenu nyinyi wenyewe.» Lakini wengi wa hawa washirikina hawaangalii wala hawazingatii ni nani anayestahiki kusifiwa na kushukuriwa , kwa hivyo ndivyo wakamshirikisha mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu.