Hakukuwa kuumbwa kwenu, wala kufufuliwa kwenu ila ni kama nafsi moja tu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kuona. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakukuwa kuwaumba nyinyi, enyi watu, na kuwafufua Siku ya Kiyama, vile ilivyo nyepesi na rahisi, isipokuwa ni kama kuumba nafsi moja na kuifufua. Hakika Mwenyezi Mungu Anayasikia maneno yenu, Anayaona matendo yenu, na Atawalipa kwa hayo.