Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Luqman 31:32

31:32
واذا غشيهم موج كالظلل دعوا الله مخلصين له الدين فلما نجاهم الى البر فمنهم مقتصد وما يجحد باياتنا الا كل ختار كفور ٣٢
وَإِذَا غَشِيَهُم مَّوْجٌۭ كَٱلظُّلَلِ دَعَوُا۟ ٱللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ فَلَمَّا نَجَّىٰهُمْ إِلَى ٱلْبَرِّ فَمِنْهُم مُّقْتَصِدٌۭ ۚ وَمَا يَجْحَدُ بِـَٔايَـٰتِنَآ إِلَّا كُلُّ خَتَّارٍۢ كَفُورٍۢ ٣٢
وَإِذَا
غَشِيَهُم
مَّوۡجٞ
كَٱلظُّلَلِ
دَعَوُاْ
ٱللَّهَ
مُخۡلِصِينَ
لَهُ
ٱلدِّينَ
فَلَمَّا
نَجَّىٰهُمۡ
إِلَى
ٱلۡبَرِّ
فَمِنۡهُم
مُّقۡتَصِدٞۚ
وَمَا
يَجۡحَدُ
بِـَٔايَٰتِنَآ
إِلَّا
كُلُّ
خَتَّارٖ
كَفُورٖ
٣٢
Na wimbi linapo wafunika kama wingu, wao humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafia dini. Lakini anapo waokoa wakafika nchi kavu, wapo baadhi yao huenda mwendo wa sawa. Wala hazikanushi Ishara zetu ila aliye khaini kafiri mkubwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na washirikina wanapopanda majahazini na mawimbi makubwa yakawazunguka pambizoni mwao kama vile mawingu na majabali, huingiwa na hofu na babaiko la kuogopa kuzama, na hapo wanamkimbilia Mwenyezi Mungu na wanamtakasia dua zao, na Anapowaokoa Akawafikisha kwenye bara, kati yao kutakua na mtu wa kati na kati asiyemshukuru Mwenyezi Mungu kikamilifu, na kati yao kutakuwa na mwenye kukanusha neema za Mwenyezi Mungu na kuzikataa. Na hakanushi aya zetu na hoja zetu zenye kutolea ushahidi ukamilifu wa uweza wetu na upweke wetu isipokuwa kila mwingi wa kuvunja ahadi, mwingi wa kukataa neema za Mwenyezi Mungu juu Yake.