Je! Mwenye kuwa na bayana kutoka kwa Mola wake Mlezi ni kama aliye pambiwa uovu wa vitendo vyake, na wakafuata pumbao lao? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Je yule aliyekuwa na ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ujuzi kuwa Yeye ni Mmoja, ni kama yule ambaye Shetani amempambia matendo yake maovu na akafuata yale ambayo nafsi yake ilimuita iyafuate ya kumuasi Mwenyezi Mungu na kumuabudu asiyekuwa Yeye bila ya hoja wala ushahidi? Hawalingani.