Hakika walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, kisha wakafa na hali ni makafiri, Mwenyezi Mungu hatawasamehe makosa yao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika ya wale waliokataa kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki Peke Yake Asiye na mshirika na wakawazuia watu na Dini Yake, kisha wakafa wakiwa katika hali hiyo, Mwenyezi Mungu Hatawasamehe, na Atawapa adhabu ikiwa ndio mateso yao kwa ukanushaji wao, na Atawafedhehesha mbele ya halaiki ya watu.