Atakughufirieni madhambi yenu, na atakuakhirisheni mpaka muda ulio wekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapo fika haucheleweshwi. Laiti mngejua! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mwenyezi Mungu Atawasamehe dhambi zenu na kuwafinikia, atawarefushia umri wenu mpaka kipindi kilichokadiriwa katika ujuzi wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Kwani kifo kikija hakicheleweshwi kabisa. Lau mngalijua hilo mngalifanya haraka kuamini na kutii.»