Hao ndio watakao lipwa makao ya juu kwa kuwa walisubiri, na watakuta humo maamkio na salamu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Hao waja wa Mwingi wa rehema, waliosifika kwa sifa zilizopita, watalipwa majumba ya Peponi ya juu kabisa, kwa rehema ya Mwenyezi Mungu na kwa sababu ya uvumilivu wao juu ya kufanya matendo ya utiifu, na watalakiwa humo Peponi kwa maamkizi na salamu kutoka kwa Malaika, na watakuta maisha mema na kusalimika na maafa,