Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
050

Qaf 50:23 وقال قرينه هاذا ما لدي عتيد ٢٣

50:23
وَقَالَ
قَرِينُهُۥ
هَٰذَا
مَا
لَدَيَّ
عَتِيدٌ
٢٣
Na mwenzake atasema: Huyu niliye naye mimi kesha tayarishwa. 1
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis

Na Malaika mwandishi mwenye kumtolea ushahidi atasema, «Haya ndiyo niliyonayo kutoka kwenye rikodi ya matendo yake. Nayo imetayarishwa, imehifadhiwa na ipo hapa kwangu.»
Na Malaika mwandishi mwenye kumtolea ushahidi atasema, «Haya ndiyo niliyonayo kutoka kwenye rikodi ya matendo yake. Nayo imetayarishwa, imehifadhiwa n…
Zaidi Tafsir

Soma Maudhui Yanayohusiana

Sura 50, Ukurasa 519, Juzuu 26

16. Na hakika tumemuumba mtu, nasi tunayajua yanayo mpitikia katika nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake. 17. Wanapo pokea wapokeaji wawili, wanao kaa kuliani na kushotoni. 18. Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari. 19. Na uchungu wa kutoka roho utamjia kwa haki. Hayo ndiyo uliyo kuwa ukiyakimbia. 20. Na litapulizwa baragumu. Hiyo ndiyo Siku ya Miadi. 21. Na kila nafsi itakuja na pamoja nayo mchungaji na shahidi. 22. (Aambiwe): Kwa hakika ulikuwa umeghafilika na haya; basi leo tumekuondolea pazia lako, na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali. 23. Na mwenzake atasema: Huyu niliye naye mimi kesha tayarishwa. 24. Mtupeni katika Jahannamu kila kafiri mwenye inda, 25. Akatazaye kheri, arukaye mipaka, mwenye kutia shaka, 26. Aliye weka mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni katika adhabu kali. 27. Mwenzake aseme: Ee Mola wetu Mlezi! Sikumpoteza mimi, bali yeye mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali. 28. (Mwenyezi Mungu) aseme: Msigombane mbele yangu. Nilikuleteeni mbele onyo langu. 29. Mbele yangu haibadilishwi kauli, wala Mimi siwadhulumu waja wangu.

- Swahili Translation - Ali Muhsin Al-Barwani

Maelezo na Tafakari

Hakuna tafakari zilizokaguliwa kwa aya hii

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia