Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Saba 34:11

34:11
ان اعمل سابغات وقدر في السرد واعملوا صالحا اني بما تعملون بصير ١١
أَنِ ٱعْمَلْ سَـٰبِغَـٰتٍۢ وَقَدِّرْ فِى ٱلسَّرْدِ ۖ وَٱعْمَلُوا۟ صَـٰلِحًا ۖ إِنِّى بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌۭ ١١
أَنِ
ٱعۡمَلۡ
سَٰبِغَٰتٖ
وَقَدِّرۡ
فِي
ٱلسَّرۡدِۖ
وَٱعۡمَلُواْ
صَٰلِحًاۖ
إِنِّي
بِمَا
تَعۡمَلُونَ
بَصِيرٞ
١١
(Tukamwambia:) Tengeneza nguo za chuma pana, na kadiria sawa katika kuunganisha. Na tendeni mema. Hakika Mimi nayaona vyema mnayo yatenda. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
(Na tulikwambia, ewe Dāwūd,) «Tengeneze nguo za chuma zilizotimia na zilizo pana, na ukadirie vipimo vya misumari katika vikuku vya kuunganisha nguo hizo za chuma, na usikifanye kikuku kuwa kidogo kwani kitakuwa dhaifu, na kwa hivyo hizo nguo za chuma hazitaweza kumkinga (mwenye kuzivaa). Na usizifanye kubwa zikawa nzito kwa mwenye kuzivaa. Na ufanye, ewe Dāwūd, wewe na watu wako, vitendo vya kumtii Mwenyezi Mungu, kwani mimi kwa mnayoyafanya ni Mwenye kuyaona, hakifichamani kwangu kitu chochote katika hivyo.»