Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Saba 34:14

34:14
فلما قضينا عليه الموت ما دلهم على موته الا دابة الارض تاكل منساته فلما خر تبينت الجن ان لو كانوا يعلمون الغيب ما لبثوا في العذاب المهين ١٤
فَلَمَّا قَضَيْنَا عَلَيْهِ ٱلْمَوْتَ مَا دَلَّهُمْ عَلَىٰ مَوْتِهِۦٓ إِلَّا دَآبَّةُ ٱلْأَرْضِ تَأْكُلُ مِنسَأَتَهُۥ ۖ فَلَمَّا خَرَّ تَبَيَّنَتِ ٱلْجِنُّ أَن لَّوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ ٱلْغَيْبَ مَا لَبِثُوا۟ فِى ٱلْعَذَابِ ٱلْمُهِينِ ١٤
فَلَمَّا
قَضَيۡنَا
عَلَيۡهِ
ٱلۡمَوۡتَ
مَا
دَلَّهُمۡ
عَلَىٰ
مَوۡتِهِۦٓ
إِلَّا
دَآبَّةُ
ٱلۡأَرۡضِ
تَأۡكُلُ
مِنسَأَتَهُۥۖ
فَلَمَّا
خَرَّ
تَبَيَّنَتِ
ٱلۡجِنُّ
أَن
لَّوۡ
كَانُواْ
يَعۡلَمُونَ
ٱلۡغَيۡبَ
مَا
لَبِثُواْ
فِي
ٱلۡعَذَابِ
ٱلۡمُهِينِ
١٤
Na tulipo mhukumia kufa, hapana aliye wajuulisha kufa kwake ila mnyama wa ardhi aliye kula fimbo yake. Na alipo anguka majini walitambua lau kuwa wangeli jua ya ghaibu wasingeli kaa katika adhabu hiyo ya kufedhehesha. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Tulipopitisha kuwa Sulaymān afe, hakuna kilichowafahamisha majini juu ya kifo chake isipokuwa mchwa kuila fimbo yake ambayo alikuwa ameitegemea, basi Sulaymam akaanguka chini, na hapo majini wakajua kwamba wao lau walikuwa wanajua ghaibu hawangalikaa kwenye adhabu yenye kudhalilisha na kazi ngumu kumfanyia Sulaymān, kwa wao kudhania kuwa yeye ni katika walio hai. Katika hii aya kuna kubatilisha itikadi ya baadhi ya watu kwamba majini wanayajua yasiyoonekana. Kwani lau wao wangaliyajua yasiyoonekana wangalijua kifo cha Sulaymān, amani imshukie, na hawangalikaa kwenye adhabu yenye kunyongesha.