Na walikadhibisha walio kuwa kabla yao. Na hawakufikilia hata sehemu moja katika kumi ya tulivyo wapa hao. Nao waliwakadhibisha Mitume wangu. Basi kuangamiza kwangu kulikuwa namna gani! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na walikanusha wale waliokuwa kabla yao, kama vile 'Ād na Thamūd, Na watu wa Makkah hawakufikia ushuri wa kile tulichowapa ummah waliopita cha nguvu, wingi wa mali, umri mrefu na neema nyiginezo, na tukawaangamiza. Basi angalia, ewe Mtume! Ni namna gani yalivyokuwa makemeo yangu na adhabu yangu kwao?