Mwenyezi Mungu akamwambia: Ewe Iblisi! Kipi kilicho kuzuia kumt'ii yule niliye muumba kwa mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mwenyezi Mungu Akamwambia Iblisi, «Ni lipi lililokukataza kumsujudia yule niliyemkirimu nikamuumba kwa mikono yangu miwili? Je, umemfanyia kiburi Ādam au umekuwa ni miongoni mwa wale waliomfanyia kiburi Mola wako?» Katika aya hii pana kumthibitishia Mwenyezi Mungu, Mwenye kheri nyingi na kutukuka, sifa ya mikono miwili, kwa namna inayolingana na Yeye, kutakasika ni Kwake.