Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
038

Sad 38:8 اانزل عليه الذكر من بيننا بل هم في شك من ذكري بل لما يذوقوا عذاب ٨

38:8
أَءُنزِلَ
عَلَيۡهِ
ٱلذِّكۡرُ
مِنۢ
بَيۡنِنَاۚ
بَلۡ
هُمۡ
فِي
شَكّٖ
مِّن
ذِكۡرِيۚ
بَل
لَّمَّا
يَذُوقُواْ
عَذَابِ
٨
Ati yeye tu ndiye aliye teremshiwa mawaidha peke yake katika sisi? Lakini hao wana shaka na mawaidha yangu, bali hawajaionja adhabu yangu. 1
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis

«Je, amehusishwa Muhammad peke yake kwa kuteremshiwa Qur’ani bila ya sisi?» Bali wao wako kwenye shaka ya kuwa mimi nimekuletea wahyi wewe, ewe Mtume, na kukupa utume. Bali wao walisema hilo kwa kuwa hawajaonja adhabu ya Mwenyezi Mungu, na lau wangaliionja adhabu hawangalithubutu kusema waliyosema.
«Je, amehusishwa Muhammad peke yake kwa kuteremshiwa Qur’ani bila ya sisi?» Bali wao wako kwenye shaka ya kuwa mimi nimekuletea wahyi wewe, ewe Mtume,…
Zaidi Tafsir

Soma Maudhui Yanayohusiana

Sura 38, Ukurasa 453, Juzuu 23

1. S'ad, Naapa kwa Qur'ani yenye mawaidha. 2. Lakini walio kufuru wamo katika majivuno na upinzani . 3. Mataifa mangapi tumeyaangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa kuokoka ulikwisha pita. 4. Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anaye tokana nao wenyewe, na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo. 5. Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu. 6. Na wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu, kwani hili ni jambo lililo pangwa. 7. Sisi hatukusikia haya katika mila hii ya mwisho. Haya si chochote ila ni uzushi tu. 8. Ati yeye tu ndiye aliye teremshiwa mawaidha peke yake katika sisi? Lakini hao wana shaka na mawaidha yangu, bali hawajaionja adhabu yangu. 9. Au wanazo wao khazina za rehema za Mola wako Mlezi, Mwenye nguvu, Mpaji? 10. Au wao wana ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo kati yao? Basi nawazipande njia za kwendea huko! 11. Hao ni askari watao shindwa miongoni mwa makundi yatayo shindwa. 12. Walikanusha kabla yao kaumu ya Nuhu, na kina A'adi na Firauni mwenye majengo. 13. Na Thamud na kaumu Lut'i na watu wa Machakani. Hayo ndiyo makundi. 14. Hao wote waliwakadhibisha Mitume; basi wakastahiki adhabu yangu.

- Swahili Translation - Ali Muhsin Al-Barwani

Maelezo na Tafakari

Hakuna tafakari zilizokaguliwa kwa aya hii

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia