Hao ni watu walio kwisha pita. Watapata waliyo yachuma, nanyi mtapata mtakayo yachuma; wala hamtaulizwa nyinyi waliyo kuwa wakiyafanya wao. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Hao ni Ummah waliopita miongoni mwa wale waliowatangulia nyinyi. Wao wana amali zao, na nyinyi muna amali zenu. Wala hamtaulizwa kuhusu amali zao. Na wao hawataulizwa kuhusu amali zenu. Na kila mmoja atalipwa kulingana na aliyoyatenda. Mtu hateswi kwa kosa la yoyote mwengine. Na haimnufaishi mtu ila Imani yake na uchaji Mungu wake.