Ukikupata wema unawachukiza, na ukikusibu msiba, wao husema: Sisi tuliangalia mambo yetu vizuri tangu kwanza. Na hugeuka kwenda zao nao wamefurahi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Ewe Nbii! Unapofikiwa na furaha na ngawira, wanafiki wanasikitika, na unapopatwa na kero la kushindwa au matatizo, wanasema,»Sisi ni wenye busara na uhodari wa kupanga, tulijipangia kwa maslahi yetu kubakia nyuma na kutomfuata Muhammad.» Na hapo wanaondoka hali ya kuwa na furaha kwa waliyoyafanya na kwa mabaya yaliyokufika.