Tulipo watumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Tulipowatumia wajumbe wawili wawalinganie kumuamini Mwenyezi Mungu na kuacha kumuabudu asiyekuwa Yeye. Watu wa kijiji wakawakanusha wajumbe wawili hao tukawatilia nguvu kwa mjumbe wa tatu. Basi hao wajumbe watatu walisema kuwaambia watu wa kijiji, «Hakika sisi kwenu nyinyi,enyi watu, tumetumwa.»