Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Yasyn 36:19

36:19
قالوا طايركم معكم اين ذكرتم بل انتم قوم مسرفون ١٩
قَالُوا۟ طَـٰٓئِرُكُم مَّعَكُمْ ۚ أَئِن ذُكِّرْتُم ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌۭ مُّسْرِفُونَ ١٩
قَالُواْ
طَٰٓئِرُكُم
مَّعَكُمۡ
أَئِن
ذُكِّرۡتُمۚ
بَلۡ
أَنتُمۡ
قَوۡمٞ
مُّسۡرِفُونَ
١٩
Wakasema: Ukorofi wenu mnao wenyewe! Je! Ni kwa kuwa mnakumbushwa? Ama nyinyi ni watu walio pindukia mipaka. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Wajumbe wakasema, «Kisirani chenu na matendo yenu ya ushirikina na ya shari yako na nyinyi na yanarudishwa kwenu nyinyi. Je, nyinyi mkiwaidhiwa kwa jambo ambalo lina kheri kwenu mnajihisi mmeingiliwa na kisrani na mnatutisha kuwa mtatupiga mawe na kutuadhibu? Bali nyinyi ni watu ambao desturi yenu ni kupita kiasi katika uasi na ukanushaji.