Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Yasyn 36:8

36:8
انا جعلنا في اعناقهم اغلالا فهي الى الاذقان فهم مقمحون ٨
إِنَّا جَعَلْنَا فِىٓ أَعْنَـٰقِهِمْ أَغْلَـٰلًۭا فَهِىَ إِلَى ٱلْأَذْقَانِ فَهُم مُّقْمَحُونَ ٨
إِنَّا
جَعَلۡنَا
فِيٓ
أَعۡنَٰقِهِمۡ
أَغۡلَٰلٗا
فَهِيَ
إِلَى
ٱلۡأَذۡقَانِ
فَهُم
مُّقۡمَحُونَ
٨
Tumeweka makongwa shingoni mwao, yakawafika videvuni. Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika sisi tumewafanya hawa makafiri, ambao walionyeshwa haki wakaikataa na wakawa wakakamavu kushikilia ukafiri na kuacha kuamini, ni kama wale waliofungwa pingu shingoni mwao, ikakusanywa pamoja mikono yao pamoja na shingo zao chini ya videvu vyao, wakalazimika kuinua juu vichwa vyao. Basi wao wamefungwa na kuepushwa na kila kheri, hawaioni haki wala hawaongoki kuifuata.