Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Yunus 10:109

10:109
واتبع ما يوحى اليك واصبر حتى يحكم الله وهو خير الحاكمين ١٠٩
وَٱتَّبِعْ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيْكَ وَٱصْبِرْ حَتَّىٰ يَحْكُمَ ٱللَّهُ ۚ وَهُوَ خَيْرُ ٱلْحَـٰكِمِينَ ١٠٩
وَٱتَّبِعۡ
مَا
يُوحَىٰٓ
إِلَيۡكَ
وَٱصۡبِرۡ
حَتَّىٰ
يَحۡكُمَ
ٱللَّهُۚ
وَهُوَ
خَيۡرُ
ٱلۡحَٰكِمِينَ
١٠٩
Na wewe fuata yanayo funuliwa kwako kwa wahyi. Na vumilia mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu, na Yeye ndiye mbora wa mahakimu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na uufuate, ewe Mtume, wahyi wa Mwenyezi Mungu Aliokutumia wewe na uutumie kivitendo. Na uwe na subira katika kumtii Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na katika kujiepusha na mambo ya kumuasi na kwa kuvumilia makero ya wenye kukukera katika kuufikisha ujumbe Wake, mpaka Mwenyezi Mungu Atoe uamuzi Wake kwao na kwako. Na Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, Ndiye mbora wa kutoa uamuzi, kwa kuwa uamuzi Wake unakusanya uadilifu uliokamilika.