Basi huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu wa haki. Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu? Basi huwaje mkageuzwa? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Huyo Ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu! Yeye Ndiye kweli isiyo na shaka, Anayestahiki kuabudiwa Peke Yake, Asiye na Mshirika. Basi ni kitu gani kisichokuwa kweli isipokuwa ni upotevu? Basi vipi nyinyi mtaepushwa na kumuabudu Yeye muelekezwe kumuabudu asiyekuwa Yeye?