Je! Ndiyo wanasema ameizua? Sema: Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite (kukusaidieni) muwawezao, isipo kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnasema kweli. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Au kwani wao wanasema kwamba Muhammad ameizua hii Qur’ani yeye mwenyewe? Wao wanajua kwamba yeye ni mwanadamu kama wao. Waambie, «Basi leteni sura moja inayofanana na hii Qur’ani katika mpango wake na uongozi wake, na takeni usaidizi wa kufanya hilo kwa mnayemuweza, badala ya Mwenyezi Mungu, miongoni mwa majini na binadamu, iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu.»