Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Yunus 10:93

10:93
ولقد بوانا بني اسراييل مبوا صدق ورزقناهم من الطيبات فما اختلفوا حتى جاءهم العلم ان ربك يقضي بينهم يوم القيامة فيما كانوا فيه يختلفون ٩٣
وَلَقَدْ بَوَّأْنَا بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ مُبَوَّأَ صِدْقٍۢ وَرَزَقْنَـٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَـٰتِ فَمَا ٱخْتَلَفُوا۟ حَتَّىٰ جَآءَهُمُ ٱلْعِلْمُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِى بَيْنَهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ فِيمَا كَانُوا۟ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ٩٣
وَلَقَدۡ
بَوَّأۡنَا
بَنِيٓ
إِسۡرَٰٓءِيلَ
مُبَوَّأَ
صِدۡقٖ
وَرَزَقۡنَٰهُم
مِّنَ
ٱلطَّيِّبَٰتِ
فَمَا
ٱخۡتَلَفُواْ
حَتَّىٰ
جَآءَهُمُ
ٱلۡعِلۡمُۚ
إِنَّ
رَبَّكَ
يَقۡضِي
بَيۡنَهُمۡ
يَوۡمَ
ٱلۡقِيَٰمَةِ
فِيمَا
كَانُواْ
فِيهِ
يَخۡتَلِفُونَ
٩٣
Na hakika tuliwaweka Wana wa Is raili kikao chema, na tukawaruzuku vitu vizuri. Nao hawakukhitalifiana mpaka ilipo wafikia ilimu. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyo kuwa wakikhitalifiana. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hakika tuliwashukisha Wana wa Isrāīl mashukio mazuri yaliyoteuliwa katika miji ya Sham na Misri na tukawaruzuku riziki ya halali iliyo nzuri itokanayo na mazuri ya ardhi iliyobarikiwa. Na hawakutafautiana, katika mambo ya Dini yao isipokuwa baada ya kujiwa na ujuzi wa kuwafanya wao wawe pamoja na washikane, miongoni mwao ni yale yaliyomo ndani ya Taurati kuhusu habari ya unabii wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye. Kwa kweli, Mola wako, ewe Mtume, Atahukumu baina yao Siku ya Kiyama na Atatoa uamuzi katika yale waliokuwa wakitafautiana juu yake kuhusu mambo yako, wapate kuingia wakanushaji Motoni na Waumini Peponi.