Basi Mola wake Mlezi akamwitikia, na akamwondoshea vitimbi vyao. Hakika Yeye ni Msikizi Mjuzi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mwenyezi Mungu Akamkubalia Yūsuf maombi yake, akamwepushia kile alichotaka mke wa Kiongozi na marafiki zake kutoka kwake cha kumuasi Mwenyezi Mungu. Mwenyezi mungu Ndiye Mwenye kuyasikia maombi ya Yūsuf na maombi ya kila mwenye kuomba kati ya waja Wake, Ndiye Mwenye kuyajua matakwa yake, haja zake na kile kinachomfaa, na pia haja za viumbe Vyake vyote na yale yanayowafaa.