Na walipo ingia kwa Yusuf aliwakumbatia wazazi wake na akasema: Ingieni Misri, Inshallah, mmo katika amani. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Ya’qūb na watu wa nyumbani kwake wakatoka kuelekea Misri wakimkusudia Yūsuf. Walipofika kwake, Yūsuf aliwakumbatia wazazi wake wawili na akawaambia (wao wote), «Ingieni Misri kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu na hali mkiwa mko kwenye amani na mumeepukana na shida, ukame na kila zito.»