Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
43:15
وجعلوا له من عباده جزءا ان الانسان لكفور مبين ١٥
وَجَعَلُوا۟ لَهُۥ مِنْ عِبَادِهِۦ جُزْءًا ۚ إِنَّ ٱلْإِنسَـٰنَ لَكَفُورٌۭ مُّبِينٌ ١٥
وَجَعَلُواْ
لَهُۥ
مِنۡ
عِبَادِهِۦ
جُزۡءًاۚ
إِنَّ
ٱلۡإِنسَٰنَ
لَكَفُورٞ
مُّبِينٌ
١٥
Na wanamfanyia katika waja wake fungu. Kwa hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila aliye dhaahiri. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Na hawa washirikina wamemfanya Mwenyezi Mungu kuwa na fungu miongoni mwa waja Wake. Nako ni kule kusema kwao kuhusu Malaika kuwa ni watoto wa kike wa mwenyezi Mungu. Kwa hakika, binadamu ni mwingi wa kukanusha neema za Mola Wake Alizowaneemesha kwazo, ni mwenye kudhihirisha kukataa kwake na kukanusha kwake, anahesabu misiba na anasahau neema.