Waambie walio amini wawasamehe wale wasio zitaraji siku za Mwenyezi Mungu, ili awalipe kwa waliyo kuwa wakiyachuma. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Sema, ewe Mtume, uwaambie wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na wakamfuata Mtume Wake, wawasamehe na kuwaachilia wale ambao hawana matarajio ya malipo mema ya Mwenyezi Mungu na hawaogopi adhabu Yake wanapowakusudia Waumini kuwaudhi na kuwakera, ili Mwenyezi Mungu Awalipe washirikina hawa kwa yale waliyoyachuma duniani ya madhambi na kuwaudhi Waumini.