Watadumu humo milele. Hakika kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo makubwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Hali ya kukaa kwenye mabustani hayo ya Pepo neema hizo kikao kisicho na kikomo. Na hayo ni malipo ya yale waliyoyatanguliza ya utiifu na vitendo vyema katika maisha yao ya ulimwenguni. Hakika Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ana malipo makubwa kwa aliyeamini na akafanya mema kwa kuzifuata amri Zake na kuyaepuka Makatazo Yake.