Sema: Halitusibu ila alilo tuandikia Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mola wetu Mlinzi. Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Sema, ewe Nabii, uwaambie hao wanaovunja moyo kwa kujitoa, kwa kuwakemea na kuwaumbua, «Hakuna litakalotupata isipokuwa lile Alilolipitisha Mwenyezi Mungu juu yetu na Aliloliandika katika al-Lawḥ al-Maḥfūẓ (Ubao Uliohifadhiwa). Yeye Ndiye Mwenye kutupa ushindi juu ya maadui wetu.» Na kwa Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na wajitegemeze wale wanaoumuamini.