Basi akawalipa unaafiki kuutia nyoyoni mwao mpaka Siku watapo kutana naye, kwa sababu ya kuwa walimkhalifu Mwenyezi Mungu katika yale waliyo muahidi, na kwa sababu ya kusema kwao uwongo. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Ikawa malipo ya mambo waliyoyafanya na mwisho wao ni kwamba aliwaongezea unafiki juu ya unafiki wao, hawataweza kujisafisha nao mpaka Siku ya kuhesabiwa. Hayo ni kwa sababu ya kwenda kwao kinyume na ahadi walioitoa juu ya nafsi zao na kwa sababu ya unafiki wao na urongo wao.