Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
2:180
كتب عليكم اذا حضر احدكم الموت ان ترك خيرا الوصية للوالدين والاقربين بالمعروف حقا على المتقين ١٨٠
كُتِبَ عَلَيْكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ ٱلْمَوْتُ إِن تَرَكَ خَيْرًا ٱلْوَصِيَّةُ لِلْوَٰلِدَيْنِ وَٱلْأَقْرَبِينَ بِٱلْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى ٱلْمُتَّقِينَ ١٨٠
كُتِبَ
عَلَيۡكُمۡ
إِذَا
حَضَرَ
أَحَدَكُمُ
ٱلۡمَوۡتُ
إِن
تَرَكَ
خَيۡرًا
ٱلۡوَصِيَّةُ
لِلۡوَٰلِدَيۡنِ
وَٱلۡأَقۡرَبِينَ
بِٱلۡمَعۡرُوفِۖ
حَقًّا
عَلَى
ٱلۡمُتَّقِينَ
١٨٠
Mmeandikiwa -- mmoja wenu anapo fikwa na mauti, kama akiacha mali -- afanye wasia kwa wazazi wake na jamaa zake kwa namna nzuri inayo pendeza. Ni waajibu haya kwa wachamngu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Mwenyezi Mungu Amewafaradhia nyinyi, iwapo mmoja wenu zimedhihiri kwake alama za mauti na vitangulizi vyake, akiwa ameacha mali, atoe wasia wa sehemu ya mali yake iyende kwa wazazi wake wawili na jamaa zake alio karibu naye, pamoja na kuchunga uadilifu, asimuache masikini na akatoa wasia wake kwa tajiri, wala wasia wake usizidi thuluthi ya mali. Hiyo ni haki thabiti ambayo wenye kumcha Mwenyezi Mungu waitenda. Hii ilikuwa kabla ya kuteremka zile aya ambazo Mwenyezi Mungu aliweka fungu la kila mrith.