Yeye humpa hikima amtakaye; na aliye pewa hikima bila ya shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Mwenyezi Mungu Anampa taufiki ya usawa katika kunena na kutenda Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na yoyote ambaye Mwenyezi Mungu Amemneemesha kwa hilo, Hua Amempa kheri nyingi. Na hatakumbuka hilo na kunufaika nalo isipokuwa wenye akili zenye kung’ara kwa nuru ya Mwenyezi Mungu na uongofu Wake.