Na tulipo sema: Ingieni mji huu, na humo mle mpendapo maridhawa, na ingieni katika mlango wake kwa unyenyekevu, na semeni: Tusamehe! Tutakusameheni makosa yenu, na tutawazidishia wema wafanyao wema. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Na Kumbukeni neema yetu kwenu, tuliposema, “Ingieni mji wa Baitul Maqdis na kuleni vizuri vyake, mahali popote pa mji huo, kwa starehe. Na muwe, katika kuingia kwenu, wanyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, wadhalilifu Kwake na mseme, ‘Ewe Mola wetu, tuondolee madhambi yetu,’ tutawaitikia, tutawasamehe na kuyafanya yasitirike.” Na wenye Kufanya wema katika amali zao tutawazidishia kheri na thawabu.