Kwani hawajui kwamba Mwenyezi Mungu Anamkunjulia riziki Anayemtaka kwa kumjaribu: atashukuru au atakufuru? Na (kwani hawajui kwamba Yeye) Anambania riziki Anayemtaka kwa kumjaribu: je atavumilia au atababaika? Hakika katika kukunjulia na kubania kuna alama (za utendakazi wa Mwenyezi Mungu) kwa watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na wanaojua hekima ya Mwenyezi Mungu na rehema Yake.