Tur dağını, gölgelik gibi onların üzerlerine yükseltmiştik, onlar tepelerine düşeceğini sanmışlardı. Onlara: "Size verdiğimiz Kitap'a sıkıca sarılın, içinde olanı düşünün ki sakınanlardan olasınız" demiştik.
Tefsirler
Katmanlar
Dersler
Yansımalar
Cevaplar
Kıraat
Hadis
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi tulipoliinua jabali juu ya Wana wa Isrāīl likawa kama kwamba ni kiwingu kinachowafinika, wakawa na yakini kuwa kitawaangukia iwapo hawatazikubali hukumu zilizomo kwenye Taurati, na tukawaambia,»Chukueni tulichowapa kwa nguvu.» Yaani, fuateni kivitendo tulichowapa kwa bidii yenu, na yakumbukeni yaliyomo kwenye Kitabu chetu ya ahadi na masharti tuliyoyachukuwa kwenu kwamba mtayatekeleza yaliyomo ndani yake, ili mumche Mola wenu mpate kuokoka na mateso Yake.