Makifiri hawa ndio wale waliokuwa wakiipuuza njia ya Mwenyezi Mungu iliyolingana sawa, na wakiwazuia watu wasiifuate, na wakitaka kwamba njia ya kuifuata iwe kombo ili kusiwe na yoyote wa kuielewa; na wao, kuhusu Akhera na mambo yake, ni wenye kukanusha.