Back to Learning Plan
Lenzi Tano za Kutafakari Qur’ani
Day 1: Kufungua Vifuli vya Nyoyo Zetu kwa Kufungua Kitabu
Tunaanza kwa yakini kwamba kheri yote imo katika mawasiliano haya kutoka kwa Muumba na Mola wetu. Tunatambua kwamba jukumu letu si jingine bali kujirekebisha na kujiweka tayari ili kupokea kheri hiyo na mwongozo Wake.
“Je, Qur’ani imefungwa?”
Tutazingatia jinsi ya kutafakari Qur’ani. Lakini hatutazungumza kuhusu “kufungua” Qur’ani, kana kwamba Qur’ani imefungwa, kwa sababu moja muhimu sana: Mwenyezi Mungu hakutuambia kwamba Ameifunga Qur’ani!
Badala yake, tunajifunza kutoka katika aya moja kwamba kuna nyoyo zilizo na vifuli juu yake.
Unaweza kusoma zaidi kuhusu hilo hapa: Kufungua MOYO wako kwa ajili ya QUR’ANI (kwa lugha ya kiingereza)
“Ni vifuli vya aina gani vilivyo juu ya moyo wangu?”
Nilipotafakari aya hii, ilinifanya nijiulize:
“Ni vifuli vya aina gani ambavyo sisi waumini tunaweza kuwa navyo juu ya mioyo yetu vinavyotuzuia kuitafakari Qur’ani?”
Ikiwa situmii muda wangu na Kitabu hiki, sikipatii kipaumbele na umakini wangu, wala sitafuti kwa dhati mwongozo wake kwa ajili ya maisha yangu na dini yangu, basi huenda nikakosa kiini cha Qur’ani — hata ikiwa nina imani nacho.
(Labda tunaweza kuchukua ilhamu kutoka katika baadhi ya tafakari juu ya aya ya Qur’ani 38:29, inayotuonyesha kwamba baraka za Kitabu hiki hupatikana pale tunapotafakari na kuweka nia ya kutenda:
https://quranreflect.com/?filters=38:29-29)
“Tafakari ni nini? Na ninawezaje kutafakari?”
Natumaini kuwa umeshawishika kuhusu “kwa nini” ni muhimu kutafakari Qur'ani, ili tuweze kuendelea mara nyingine kufikiria juu ya “nini” haswa ni tafakari, na “vipi” mtu anaweza kutafakari Qur’ani.
Nitakuwa nikielezea baadhi ya mbinu muhimu ambazo kila mmoja wetu anaweza kuzitumia kadri ya uwezo wake. Hizi zinaitwa Lenzi Tano, na nitakuwa nikiwaonyesha baadhi ya mifano ya jinsi ya kuzitumia. Pia, ningependa ushiriki nasi – na usiogope kushiriki! Tazama: “Je, UNAOGOPA KUSHIRIKI?” (kwa lugha ya kiingereza)