Sign in
Sign in
Sign in
Select Language

Back to Learning Plan

Lenzi Tano za Kutafakari Qur’ani

1: Kufungua Vifuli vya Nyoyo Zetu kwa Kufungua Kitabu
2: Ninaanzaje Kutafakari Qur’ani?
3: Kichujio cha Moyo
4: Lenzi ya Maneno
5: Lenzi ya Maneno (Sehemu ya 2)
6: Lenzi ya Maneno (Sehemu ya 3)
7: Lenzi ya Ulimwengu wa Qur’ani
8: Lenzi ya Ulimwengu wa Qur’ani (Sehemu ya 2)
9: Lenzi ya Ulimwengu wa Qur’ani (Sehemu ya 3)
10: Lenzi ya Uzoefu Wangu Binafsi
11: Lenzi ya Uzoefu Wangu Binafsi (Sehemu ya 2)
12: Lenzi ya Uzoefu Wangu Binafsi (Sehemu ya 3)
13: Lenzi ya Miunganiko
14: Lenzi ya Miunganiko (Sehemu ya 2)
15: Lenzi ya Miunganiko (Sehemu ya 3)
16: Lenzi ya Mafunzo ya Jumla
17: Lenzi ya Mafunzo ya Jumla (Sehemu ya 2)
18: Lenzi ya Mafunzo ya Jumla (Sehemu ya 3) na Hitimisho

Back to Learning Plan

Lenzi Tano za Kutafakari Qur’ani

Day 5: Lenzi ya Maneno (Sehemu ya 2)

“Lenzi ya Maneno ni nini?”

Haya ni baadhi ya maswali muhimu yanayohusu Lenzi ya Maneno:

  • Lengo la aya hii ni nini, na kila sehemu yake imetamkwa kwa kusudi gani?

  • Kwa nini imetamkwa kwa namna hii mahsusi, na kwa maneno haya hasa?

  • Ni nini ninachoweza kuthamini kupitia mpangilio wa maneno na sarufi, hasa pale ambapo kuna mkazo wa ziada au vipengele vinavyotofautiana na ilivyo kawaida?

“Ni nini kinachoweza kunisaidia kutafakari kutumia Lenzi ya Maneno?”

Kuna mbinu za kutafakari aina mahsusi za mfumo wa maneno wa Qur’ani, kama vile mifano (mithali), dua, na Majina ya Mwenyezi Mungu.  Kama tulivyosema awali, lugha ya Kiarabu ni jambo muhimu sana katika kuichunguza Qur’ani kupitia maneno yake. Lakini katika somo hili fupi, nitakuonyesha ni kiasi gani unaweza kutafakari maneno hata bila ujuzi huo; bila shaka, vitabu vya Tafsir vinasaidia kwa kiwango kikubwa sana.

“Tuanze wapi?”

Hebu tuchukue sura Al-Fatihah, ambayo inastahili kutafakariwa kila siku tunapoisoma katika swala zetu. Ili tusirefushe mambo, nitatoa mifano michache tu kati ya mamia ya maswali tunayoweza kuyauliza, na jinsi yanavyotupeleka kwenye tafakari ya kina zaidi.

“Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu” (Al-ḥamdu lillāhi rabbil-‘ālamīn)

— Kwa nini Qur’ani inatumia kauli thabiti badala ya tamko binafsi kama “Ninamsifu Mwenyezi Mungu”? Kwa sababu kauli hii inasisitiza kwamba sifa zote tayari ni Zake kwa ukamilifu, bila kutegemea matamko ya mwanadamu. Hii hunifanya nihisi ukubwa na ukamilifu wa Mwenyezi Mungu ukilinganishwa na udhaifu wangu wa kueleza sifa Zake.

“Mola wa walimwengu wote” (Rabbil-‘ālamīn)

— kwa nini si “ulimwengu” mmoja tu bali walimwengu wengi? Na maana hii inaweza kupanukaje kadri maarifa yetu kuhusu ulimwengu (cosmos) unavyozidi kupanuka?

“Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu” (Ar-Raḥmān, Ar-Raḥīm)

— Kwa nini haya majina mbalimbali yamewekwa katika Sura hii muhimu? Kwa mfano ametaja Allah, Rabb, Rahman, Rahim, Malik? Na rehema ina hadhi gani maalum ambayo inasisitizwa tena na tena mwanzoni mwa takriban kila sura? 

“Mwenye kumiliki Siku ya Malipo” (Mālik Yawm ad-Dīn)

— Nini maana ya umiliki wake wa kipekee na ukuu wake katika Siku hiyo? Kuna maani gani ya matumizi ya “Yawm al-Din” ikilinganishwa na majina ya Qiyaama mengine?  

“Wewe pekee tunakuabudu na Wewe pekee tunakuomba msaada” (iyyāka na‘budu wa iyyāka nasta‘īn)

— Inamaanisha nini na nahisi vipi sasa ninavyosoma tamko hii kutoka kwangu? Pia, kwa nini iko katika wingi na si “Ninakuabudu na Ninakuomba msaada?”

“Tuongoze Njia Iliyo Nyooka” (ihdinā ṣ-ṣirāṭ al-mustaqīm)

— dalili zipi zinapatikana katika mzizi wa neno la Kiarabu mustaqīm na athari zake hapa kama sifa ya njia? Je, maneno haya  “tuongoze”, “njia”, “nyooka” yanaweza kubadilishwa kwa visawe vyao, au kuna maana mahsusi tunayoyapata kutokana na maneno haya yenyewe?

“Njia ya wale uliowaneemesha; siyo wale walio na ghadhabu juu yao*, wala wale waliopotea.” (ṣirāṭ alladhīna an‘amta ‘alayhim ghayri l-maghḍūbi ‘alayhim walā ḍ-ḍāllīn)

— tunaweza kujifunza nini kutokana na neema kuhusishwa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu, huku mambo hasi yakielezwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja au kuhusishwa na waliokosa? Ni nini tunaweza kuelewa kuhusu makundi haya matatu yanayotajwa hapa, mbali na kuyahusisha na jamii fulani kama ilivyokuja katika hadithi?

[*Tanbihi: Tafsiri nyingi husema, kwa mfano: “wale waliopata ghadhabu Yako”, ilhali matini ya Kiarabu haitaji wazi ni ghadhabu ya nani inayokusudiwa. Hilo lenyewe ni tofauti yenye maana kubwa katika maneno, ambayo mara nyingi hupotea katika tarjuma. Kwa hiyo, ingawa tunazitumia tarjuma kadri tuwezavyo, tunapaswa kukumbuka mipaka na mapungufu yake.]

Huu ni mwanzo tu wa maswali tunayoweza kuuliza, na tunaweza kugundua kwamba wanazuoni wa tafsir tayari waliuliza na kujibu maswali kama haya hapo kabla. Hoja kuu ni kwamba tafakari SI suala la kuchukua jibu la haraka, bali ni kuchukua muda kuthamini maana, na kukuza heshima na taadhima yetu kwa Mwenyezi Mungu ﷻ na Maneno Yake.

Add Reflection

Stay Connected to the Quran ❤️

Short meaningful reminders to reset, reflect and stay connected to the Quran.

Read, Listen, Search, and Reflect on the Quran

Quran.com is a trusted platform used by millions worldwide to read, search, listen to, and reflect on the Quran in multiple languages. It provides translations, tafsir, recitations, word-by-word translation, and tools for deeper study, making the Quran accessible to everyone.

As a Sadaqah Jariyah, Quran.com is dedicated to helping people connect deeply with the Quran. Supported by Quran.Foundation, a 501(c)(3) non-profit organization, Quran.com continues to grow as a free and valuable resource for all, Alhamdulillah.

Navigate
Home
Quran Radio
Reciters
About Us
Developers
Product Updates
Feedback
Help
Donate
Our Projects
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Non-profit projects owned, managed, or sponsored by Quran.Foundation
Popular Links
Duas from the Quran
Quran Verse of the Day
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
SitemapPrivacyTerms and Conditions
© 2026 Quran.com. All Rights Reserved
Contribute