Sign in
Sign in
Sign in
Select Language

Back to Learning Plan

Lenzi Tano za Kutafakari Qur’ani

1: Kufungua Vifuli vya Nyoyo Zetu kwa Kufungua Kitabu
2: Ninaanzaje Kutafakari Qur’ani?
3: Kichujio cha Moyo
4: Lenzi ya Maneno
5: Lenzi ya Maneno (Sehemu ya 2)
6: Lenzi ya Maneno (Sehemu ya 3)
7: Lenzi ya Ulimwengu wa Qur’ani
8: Lenzi ya Ulimwengu wa Qur’ani (Sehemu ya 2)
9: Lenzi ya Ulimwengu wa Qur’ani (Sehemu ya 3)
10: Lenzi ya Uzoefu Wangu Binafsi
11: Lenzi ya Uzoefu Wangu Binafsi (Sehemu ya 2)
12: Lenzi ya Uzoefu Wangu Binafsi (Sehemu ya 3)
13: Lenzi ya Miunganiko
14: Lenzi ya Miunganiko (Sehemu ya 2)
15: Lenzi ya Miunganiko (Sehemu ya 3)
16: Lenzi ya Mafunzo ya Jumla
17: Lenzi ya Mafunzo ya Jumla (Sehemu ya 2)
18: Lenzi ya Mafunzo ya Jumla (Sehemu ya 3) na Hitimisho

Back to Learning Plan

Lenzi Tano za Kutafakari Qur’ani

Day 2: Ninaanzaje Kutafakari Qur’ani?

“Kuna tofauti gani kati ya tadabbur na tafsiri?”

Kuna mkanganyiko mkubwa kuhusu maana halisi ya kutafakari Qur’ani, jambo ambalo kwa Kiarabu mara nyingi huitwa TADABBUR.

Tunajua kwamba TADABBUR si sawa na TAFSIR. Tafsir ni taaluma ya kielimu inayohusisha kufafanua maana za Qur’ani. Hakuna aya katika Qur’ani inayowaamuru watu wote kufanya tafsir, lakini kuna aya nyingi zinazosisitiza umuhimu wa tadabbur.

“Ni nani anayepaswa kutafakari Qur’ani?”

Tafakari ni kwa ajili ya kila mmoja wetu — kuanzia mwanazuoni mkubwa kabisa hadi mimi na wewe. Ni njia ya kuipokea Qur’ani kwa umakini wa akili na wa moyo, na kuruhusu ujumbe wake utuathiri.

Sio swali la:

“Qur’ani inamaanisha nini?”

bali ni:

“Hii aya inamaanisha nini katika maisha YANGU?”
“Hii aya Ina umuhimu gani katika maisha YANGU?”

“Nitafichua nini ninapotafakari?”

Kutafakari huanza kwa kuangalia mwonekano dhahiri wa aya, kisha kuzama ndani zaidi. Wakati huo huo, tafakuri humaanisha pia kuzama ndani ya nafsi zetu.

Katika pande zote mbili — ndani ya Qur’ani na ndani ya nafsi — tunafichua ukweli ambao pengine tulikuwa tunaujua tayari, lakini tulihitaji kuuthamini na kuukumbuka upya.

Hili ni tendo la uaminifu wa imani linaloanza kwa yakini kamili kwamba haya ni maneno ya Muumba wangu, Mola wangu na Mwelekezi wangu. Hakuna upotovu katika maneno Yake, wala hakuna chochote kilichopo bila hekima kamilifu.

“Je, itakuwaje kama mimi si mzuri katika kutafakari?”

Soma tafakari nzuri (ya kiingereza) kuhusu aya hii hapa:
“Fake it ’til you Make it”

Ili tujinyenyekeze na kuruhusu Wahyi utubadilishe, tunahitaji kukuza ujuzi wa tafakuri. Huu si ujuzi wa kuzaliwa nao tu, bali ni jambo la kujifunza na kulilea. Ni aina ya uelewa unaozidi ule wa herufi na sauti.

Hivyo basi, tutakuwa tukizingatia maana na athari zake, na kozi hii itakuletea muhtasari wa stadi muhimu kwa mfumo wa Lenzi Tano. Ukishajua kuzitumia, unaweza kuanza katika kiwango cha msingi kabisa na kupanda hatua kwa hatua.

“Lenzi hizi tano ni zipi?”

Tunao Lenzi ya:

  1. Maneno (yaliyotumika au hayakutumika) 

  2. Ulimwengu wa Qur’ani

  3. Uzoefu Binafsi

  4. Miunganiko (kati ya ayah au sura za Qur'ani)

  5. Mafunzo ya Jumla

Lakini kabla hatujafika huko, kuna jambo muhimu sana la kushughulikia katika somo linalofuata… basi endelea kuwa nasi.

Add Reflection

Stay Connected to the Quran ❤️

Short meaningful reminders to reset, reflect and stay connected to the Quran.

Read, Listen, Search, and Reflect on the Quran

Quran.com is a trusted platform used by millions worldwide to read, search, listen to, and reflect on the Quran in multiple languages. It provides translations, tafsir, recitations, word-by-word translation, and tools for deeper study, making the Quran accessible to everyone.

As a Sadaqah Jariyah, Quran.com is dedicated to helping people connect deeply with the Quran. Supported by Quran.Foundation, a 501(c)(3) non-profit organization, Quran.com continues to grow as a free and valuable resource for all, Alhamdulillah.

Navigate
Home
Quran Radio
Reciters
About Us
Developers
Product Updates
Feedback
Help
Donate
Our Projects
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Non-profit projects owned, managed, or sponsored by Quran.Foundation
Popular Links
Duas from the Quran
Quran Verse of the Day
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
SitemapPrivacyTerms and Conditions
© 2026 Quran.com. All Rights Reserved
Contribute