Sign in
Sign in
Sign in
Select Language

Back to Learning Plan

Mwokozi: Masomo yenye Athari Kubwa Kutoka Surah Al-Mulk

1: Mfalme wa Wafalme Wote
2: Ukamilifu wa Uumbaji Wake
3: Onyo Ambalo Hatuwezi Kulipuuza
4: Yule Anayekujua Zaidi
5: Ardhi Iliyo Chini ya Miguu Yako
6: Mafunzo Kutoka kwa Waliokataa Ukweli
7: Kabla Maji Kudidimia Ardhini

Back to Learning Plan

Mwokozi: Masomo yenye Athari Kubwa Kutoka Surah Al-Mulk

Day 4: Yule Anayekujua Zaidi

Mada: Maarifa, rehema na ulinzi wa Allah kwa waumini.

Aya za Qur’ani

Somo na Tafakari

Baada ya taswira za kutisha za Moto wa Jahannamu katika aya za awali, Mwenyezi Mungu anaelekeza mawazo yetu kwa kundi tofauti: wale wanaomwogopa bila kumwona. Hawa ni watu ambao mioyo yao imejaa ufahamu wa Mwenyezi Mungu, hata wakati hakuna mtu mwingine anayewaangalia. Wanaahidiwa mambo mawili: msamaha wa mapungufu yao na thawabu kubwa: Pepo.

Hofu hii kwa Mwenyezi Mungu si hofu inayopooza, bali ni heshima inayotokana na upendo na ufahamu. Inatokamana na hamu ya muumini ya kutomchukiza na kutomuudhi Mola wake. Ni ufahamu kwamba Mwenyezi Mungu yuko pamoja nawe kila mahali na wakati: sokoni na nyumbani kwako, katika unachosema kwa sauti na kile unachoficha ndani ya moyo wako.

Aya ya 13 ni ukumbusho wenye nguvu kwamba hakuna wazo lililo dogo sana hadi kuponyoka ujuzi Wake. Iwe ni nia zetu zilizofichwa, au kinyongo, au upendo, au hata matumaini yetu, yote yanawekwa wazi mbele Yake. Hili linaweza kutia hofu ikiwa mioyo yetu imepotoka. Lakini inafariji sana wakati nia zetu ni safi; jambo ambalo kwamba halieleweki na wengine. Yule anayekujua vyema si mtu aliye karibu nawe, bali ni Muumba wako.

Kisha Mwenyezi Mungu anauliza katika aya ya 14, katika swali lisilo dai jibu: "Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?" Ni mimi na wewe tunaosahau uwezo wake; Yeye ana uwezo wa vitu vyote! Kama alivyotaja mbeleni. Mungu yule yule aliyeumba mbingu bila dosari na kila seli mwilini mwako kwa uzuri wa kipekee hakika anajua hali ya roho yako. Na Yeye ni "Al-Latif" (Latifu kuliko wote): anayejua maelezo bora ya mapambano yako, na "Al-Khabeer" (Mwenye Kujua Yote): anayejua kila hali unayokabiliana nayo.

Kiini cha Jambo: Hakuna wakati ambao hauonekani. Allah anakuona. Kila kitendo kisichoonekana cha uvumilivu, kila sala ya kimya kimya, kila mapambano yaliyofichwa hurekodiwa na Yule anayekujua vizuri zaidi kuliko unavyojijua mwenyewe, na Yeye hulipa ipasavyo.

Hadith ya Mtume (Rehema na amani zimshukie)

Mtume (Rehema na amani zimshukie) alisema:
“Hakika Mwenyezi Mungu haangalii sura au utajiri wenu, bali anaangalia mioyo yenu na matendo yenu.”
(Sahih Muslim, Hadith 2564)

Usisome tu, bali tenda…

Leo fanya tendo jema moja la siri, baina yako na Allah pekee, na weka nia kwamba limefanywa kwa ajili yake tu.

Jinsi inavyosaidia:

  • Huimarisha ikhlas (ukweli wa nia).
  • Hujenga uhusiano wa kibinafsi na Mwenyezi Mungu.
  • Hulinda moyo kutokana na kujionyesha (riya).

Dua

اللَّهُمَّ اجْعَلْ سَرِيرَتِي خَيْرًا مِنْ عَلَانِيَتِي

Allahumma aj‘al sareeratee khayran min ‘alaaniyatee
“Ee Mwenyezi Mungu, fanya utu wangu wa ndani uwe bora kuliko mwonekano wangu wa nje.”

Tafakari haya:

Unapokumbuka kwamba Mwenyezi Mungu anajua siri za ndani kabisa za moyo wako, je, ni vipi utabadilisha namna unavyoishi siku yako?

Add Reflection

Stay Connected to the Quran ❤️

Short meaningful reminders to reset, reflect and stay connected to the Quran.

Read, Listen, Search, and Reflect on the Quran

Quran.com is a trusted platform used by millions worldwide to read, search, listen to, and reflect on the Quran in multiple languages. It provides translations, tafsir, recitations, word-by-word translation, and tools for deeper study, making the Quran accessible to everyone.

As a Sadaqah Jariyah, Quran.com is dedicated to helping people connect deeply with the Quran. Supported by Quran.Foundation, a 501(c)(3) non-profit organization, Quran.com continues to grow as a free and valuable resource for all, Alhamdulillah.

Navigate
Home
Quran Radio
Reciters
About Us
Developers
Product Updates
Feedback
Help
Donate
Our Projects
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Non-profit projects owned, managed, or sponsored by Quran.Foundation
Popular Links
Duas from the Quran
Quran Verse of the Day
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
SitemapPrivacyTerms and Conditions
© 2026 Quran.com. All Rights Reserved
Contribute