Al-An-Am 6:110 ونقلب افيدتهم وابصارهم كما لم يومنوا به اول مرة ونذرهم في طغيانهم يعمهون ١١٠
وَنُقَلِّبُ
أَفۡـِٔدَتَهُمۡ
وَأَبۡصَٰرَهُمۡ
كَمَا
لَمۡ
يُؤۡمِنُواْ
بِهِۦٓ
أَوَّلَ
مَرَّةٖ
وَنَذَرُهُمۡ
فِي
طُغۡيَٰنِهِمۡ
يَعۡمَهُونَ
١١٠
Nasi twazigeuza nyoyo zao na macho yao. Kama walivyo kuwa hawakuamini mara ya kwanza, tunawaacha katika maasi yao wakitangatanga. 1
Soma Tafsir
Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis
Na tutazigeuza nyoyo zao na macho yao, tuweke kizuizi baina yake na kunufaika na alama za Mwenyezi mungu, wasiziamini kama walivyokuwa hawakuziamini aya za Qur’ani zilipoteremka kwa mara ya kwanza, na tutawaacha wao wameduwaa katika kumuasi kwao Mwenyezi Mungu, hawaongoki kwenye haki na usawa.
Na tutazigeuza nyoyo zao na macho yao, tuweke kizuizi baina yake na kunufaika na alama za Mwenyezi mungu, wasiziamini kama walivyokuwa hawakuziamini a…